Skip to main content

SERA ZA FARAGHA



💠 Taarifa zako tunazo hifadhi katika App hii ni kwa ajili ya utambulisho wako kwa watumiaji wengine wa Uislamu wetu App katika sehemu za video na Chat, hii itasaidia kwa wepesi baina ya waislamu kutambuana kwa majina yetu na kupeana nasaha na kukumbushana mambo yahusuyo dini yetu. 

💠 Hatuombi wala kuhifadhi taarifa zako nyeti na pia tumeweka chaguzi kwenye baadhi ya taarifa ili muislamu awe huru kujitambulisha kwa taarifa hiyo au laa, mfano wa taarifa hizo ni Umri na maelezo yako.

💠 App hii kwa sasa haijaruhusu kutuma ujumbe binafsi kwa mtumiaji mwingine, na lengo ni kuepusha fitna baina yetu(Wanaume vs wanawake)

💠 Ikiwa lengo la chat ni kupeana nasaha na kukumbushana, hivyo hairuhusiwi mtu kutoa maneno ya chuki, dharau, matusi au kukufurisha pasina haki na dalili

💠 Mtume muhammad(Sala na salamu ziwe juu yake) ametufundisha kuwa, waislamu ni kama jengo moja..... kwa maana ya undugu wenye kushikamana kama jengo linavyojishikilia na nguzo kwa kutegemeana, Hivyo kauli mzuri baina yetu ndio msingi wetu wa kupendana. 


       KWA KUSANIKISHA NA KUTUMIA UISLAMU WETU APP UNAKUBALI KUWA:
------------------------------------------
1. Hutatoa maneno ya rugha chafu na ya kuchukiza kwa ndugu zako watumiaji

2.Huta tuma video/picha iliyo na taarifa za ulongo na Uzushi na mauzui machafu

3.Huta weka picha isiyo na maadili kwa misingi ya kiislamu katika kiungo chako(Profile picture)

4. Unakubali kuwa, endapo itathibitishwa kuwa umefanya miongoni mwa mambo hayo juu, Utaondolewa na hutaweza tena kutumia App hii. 

**Muislamu unaombwa kumtolea taarifa yeyote atakaye fanya kinyume, kwa kubonyeza alama ya alert kwenye profile yake**